# Lakini Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu Hii ina maana ya namna Yahwe alivyomtunza Yusufu na kuwa mema kwake. "Lakini Yahwe alikuwa mwema kwa Yusufu" au "Lakini Yahwe alimtunza Yusufu" # Akampa kibali mbele ya mlinzi wa gereza Hii ina maana Yahwe alisababisha mlinzi wa gereza kumkubali Yusufu na kumtendea wema. "Yahwe alisababisha mlinzi wa gereza kufurahishwa na Yusufu" # mlinzi wa gereza "msimamizi wa gereza" au "mtu mwenye usamamizi na gereza" # akawaweka mikononi mwa Yusufu Hapa "mkononi" unawakilisha nguvu ya Yusufu au uaminifu. "kumweka Yusufu juu ya" # Chochote walichokifanya, kilikuwa chini ya uangalizi wa Yusufu "Yusufu alikuwa mwanaglizi wa kila kitu walichofanya pale" # kwa sababu Yahwe alikuwa pamoja naye Hii ina maana ya jinsi Yahwe alivyomsaidia Yusufu na kumuongoza. "kwa sababu Yahwe alimuongoza Yusufu" # Yahwe akafanikisha kila alichokifanya. "Yahwe alisababisha kila kitu ambacho Yusufu alifanya kufanikiwa"