# Ikawa "Na kwa hiyo". Msemo huu unatumika kuweka alama ya tukio jipya katika simulizi. # bwana wake "Bwana wake Yusufu". Hii ina maana ya Potifa. Taarifa hii inaweza kuwekwa wazi. "Bwana wake Yusufu, Potifa" # aliposikia maelezo aliyoambiwa na mkewe "alimsikiliza mke wake akimuelezea kwake". Neno "wake" na "kwake" hapa yana maana ya Potifa. # alikasirika sana "Potifa akawa na hasira sana" # mahali walipowekwa wafungwa wa mfalme Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mahali ambapo mfalme huweka wafungwa wake" # Akawa pale "Yusufu alikaa pale"