# bwana wake "Bwana wa Yusufu." Hii ina maana ya Potifa. # Akamwambia maelelezo haya "Alielezea namna hii" # uliyemleta kwetu Neno hili "kwetu" ina maana ya Potifa, mke wake, na inamaanisha nyumba yake yote. # aliingia kunidhihaki "alikuja ndani kunifanya mpumbavu". Hapa neno "dhihaki" ni tafisida ya "kumkamata na kulala naye". "alikuja nilipokuwepo na akajaribu kunilazimisha nilale naye" # Ikawa "Kisha". Mke wa Potifa anatumiamsemo huu kuweka alama ya tukio linalofuata katika habari anayomwambia kuhusu Yusufu kujaribu kulala naye. # akakimbia nje "alikimbia haraka nje ya nyumba"