# Alizungumza na Yusufu siku baada ya siku Hii ina maana ya kwamba aliendelea kumuuliza kulala naye. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Aliendelea kumuuliza Yusufu alale naye" # kuwa naye "kuwa karibu naye" # Ikawa "Na kwa hiyo". Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya sehemu mpya ya tukio katika simulizi. # Hakuna mtu yeyote wa nyumbani "hakuna mwanamume yeyote aliyefanya katika nyumba" # akakimbia, na kutoka nje "na akakimbia nje haraka" au "na kwa haraka akakimbia nje ya nyumba"