# Muda ukafika Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi. # tazama Neno "tazama" linatuamsha kwa mshtuko ya kwamba Tamari alikuwa amebeba mapacha, ambayo haikujulikana awali. # Muda wake wa kujifungua ukafika Msemo huu "ukafika" unaweka alama kwa tukio muhimu katika simulizi. # mmoja akatoa mkono "mmoja wa watoto akatoa mkono wake nje" # mkunga Huyu ni mtu ambaye humsaidia mwanamke anayezaa mtoto. # kitambaa cha rangi ya zambarau "kitambaa cha rangi nyekundu iliyoiva" # katika mkono wake "kuzunguka kifundo cha mkono wake"