# Shua Hili ni jina la mwanamume. # Yuda akafarijika na "Yuda alipokuwa haombolezi, ali" # wakatao kondoo wake manyoya huko Timna "Timna, ambapo wanamume wake walikuwa wakinyoa manyoya ya kondoo" # Timna ... Enaimu Haya ni majina ya mahali. # yeye na rafiki yake, Hira Mwadulami "Rafiki yake Hirami, kutoka Adulami, alikwenda naye" # Hira Mwadulami "Hira" ni jina la mwanamume, na "Adulami" ni jina la kijiji ambapo aliishi. # Tamari akaambiwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu akamwambia Tamari" # Tazama, mkweo mkweo - "Sikiliza". Hapa neno "tazama" linatumika kushika nadhari ya Tamari. # mkweo mkweo - "baba wa mume wako" # ya ujane "ambayo wajane huvaa" # ushungi kitambaa chembamba sana kinachotumika kufunika kichwa na uso wa mwanamke. # na akajifunika Hii ina maana alijificha kwa nguo yake ili kwamba watu wasiweze kumtambua. Kitamaduni, sehemu za nguo za wanawake zilikuwa kubwa walizojizungushia nazo. "na akajifunika na kitambaa chake ili watu wasiweze kumtambua" # kando ya njia "kando ya barabara" au "njiani" # hakupewa kuwa mke wake Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yuda hakupatiwa kwa Shela kuwa mke"