# kwa Waishmaeli "kwa wanamume hawa ambao ni vizazi vya Ishmaeli" # tusiweke mikono yetu juu yake Hii ina maana ya kutomdhuru au kumjeruhi. "msimuumize" # ni ndugu yetu, nyama yetu Neno la "nyama" ni lugha nyingine lenye maana ya ndugu. "ni ndugu wetu wa damu" # ndugu zake wakamsikiliza "Kaka zake na Yuda walimsikiliza" au "Kaka zake Yuda walikubaliana naye" # Kimidiani ... Waishmaeli Majina yote mawili yana maana ya kundi moja la wafanyabiashara ambao ndugu zake Yusufu walikutana nao. # kwa vipande ishirini vya fedha "kwa bei ya vipande 20 vya fedha" # wakamchukua Yusufu mpaka Misri "wakampeleka Yusufu Misri"