# Je ndugu zako hawalichungi kundi huko Shekemu? Israeli anatumia swali kuanza mazungumzo. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Ndugu zako wanachunga kundi huko Shekemu". # Njoo Hapa inasemekana ya kwamba Israeli anamuomba Yusufu kujiandaa kuondoka kuonana na ndugu zake. "Jiandae" # nipo tayari Yupo tayari kuondoka. "Nipo tayari kuondoka" # Akamwambia "Israeli akamwambia Yusufu" # uniletee neno Israeli anamtaka Yusufu kurudi na kumuambia kuhusu kaka zake na hali ya mifugo. "njoo uniambie utakakikuta" au "niletee taarifa" # kutoka katika bonde "kutoka bondeni"