# Basi Neno hili linatumika hapa kuweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Israeli na Yusufu. # akampenda Hii ina maana ya upendo wa kindugu au upendo wa kirafiki au kifamilia. Huu ni upendo wa kawaida wa binadamu kati ya marafiki na ndugu. # wa uzee wake Hii ina maana ya kwamba Yusufu alizaliwa wakati Israeli alikuwa mzee. "aliyezaliwa wakati Israeli alipokuwa mtu mzee" # Akamshonea "Israeli alimshonea Yusufu" # vazi zuri "joho zuri" # hawakuongea naye vema. "hawakuweza kuongea kwa namna ya upole kwake"