# Hivi ndivyo vizazi vya Esau Sentensi hii inatambulisha habari ya vizazi vya Esau katika Mwanzo 36:9-43. "Hii ni habari ya vizazi vya Esau" # katika nchi ya mlima Seiri Hii ina maana ya kwamba waliishi katika nchi ya mlima wa Seiri. Maana kamili ya hii inaweza kuwekwa wazi. "aliyeishi katika mlima wa nchi ya Seiri" # Elifazi ... Reueli Haya ni majina ya wana wa Esau. # Ada ... Basemathi Haya ni majina ya wake wa Esau. # Temani, Omari, Zefo, Gatamu, na Kenazi ... Amaleki Haya ni majina ya wana wa Elifazi. # Timna Hili ni jina la suria wa Elifazi.