# Hivi ndivyo vizazi vya Esau (aliyeitwa pia Edomu) "Hivi ndivyo vizazi vya Esau, ambaye pia anaitwa Edomu". Sentensi hii inatambulisha habari ya vizazi vya Esau katika Mwanzo 36:1-8. "Hii ni habari ya vizazi vya Esau, ambaye pia anaitwa Edomu" # Ada ... Oholibama Haya ni majina ya wake wa Esau. # Eloni Mhiti "Eloni kizazi cha Hethi" au "Eloni uzao wa Hethi". Hili ni jina la mwanamume. # Ana ... Zibeoni ... Nebayothi Haya ni majina ya wanamume. # Mhivi Hii ina maana ya kikundi kikubwa cha watu. # Basemathi Hili ni jina la mke mmoja wa Esau. # Nebayothi Hili ni jina la mtoto mmoja wa kiume wa Ishmaeli.