# Efrathi Hili ni jina lingine la mji wa Bethelehemu. # akashikwa na uchungu "Alikuwa na wakati mgumu wakati alipokuwa akimzaa mtoto" # Alipokuwa katika utungu mzito zaidi "Uchungu ulipokuwa katika hatua mbaya zaidi" # mkunga mtu anayemsaidia mwanamke anapojifungua mtoto # Hata alipokaribia kufa, kwa pumzi yake ya mwisho "pumzi yake ya mwisho" ni pumzi ya mwisho ya mtu kabla mtu hajafa. "Hata kabla hajafa, alipovuta pumzi yake ya mwisho" # Benoni "Jina la Benoni lina maana ya "mtoto wa majonzi yangu"" # Benyamini Watafsiri wanaweza kuweka maandishi mafupi yasemayo "Jina la Benyamini lina maana ya "mtoto wa mkono wa kuume". Msemo wa "mkono wa kulia" unalenga sehemu yenye upendeleo maalumu. # na kuzikwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "na wakamzika" # katika njia "pembeni mwa barabara" # ndiyo alama ya kaburi la Raheli hata leo "inaweka alama juu ya kaburi la Raheli mpaka siku hii" # hata leo "mpaka wakati huu wa leo." Hii ina maana hadi wakati ambapo mwandishi alikuwa akiandika haya.