# Luzu Hili ni jina la mji. # El Betheli "Jina la El Betheli lina maana ya "Mungu wa Betheli" # Mungu alikuwa amejifunua kwake "pale Mungu alijifunua kwa Yakobo" # Debora Hili ni jina la mwanamke. # mlezi wa Rebeka Mlezi ni mwanamke ambaye humtunza mtoto wa mwanamke mwingine. Mlezi aliheshimika na alikuwa muhimu sana kwa familia. # Akazikwa chini kutoka Betheli Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Walimzika chini kutoka Betheli" # chini kutoka Betheli Msemo "chini kutoka" unatumika kwa sababu walimzika katika eneo ambalo lilikuwa chini kwa mwinuko kuliko Betheli. # Aloni Bakuthi. "Jina la Aloni Bakuthi lina maana ya "Mwaloni ambapo kuna maombolezo"