# Bwana wangu anajua Hii ni njia ya upole na maalumu ya kumhusu Esau. "Wewe, bwana wangu, unajua" # watoto ni wadogo Maana inaweza kuwekwa wazi zaidi. "watoto ni wadogo sana kusafiri haraka" # Ikiwa watapelekwa kwa haraka hata siku moj Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "tukiwalazimisha kwenda haraka sana hata kwa siku moja" # Tafadhari bwana wangu na amtangulie mtumishi wake Hii ni njia ya upole na maalumu ya Yakobo kujitaja mwenyewe. "Bwana wangu, mimi ni mtumishi wako. Tafadhali nenda mbele yangu" # kwa kadili ya mifugo iliyo mbele yangu "kwa kasi ya wanyama naowatunza wanaweza kwenda" # Seiri Hili ni eneo lenye milima katika eneo la Edomu.