# mpaka alfajiri "mpaka alfajiri" # nyonga "kiungo cha paja". Hii ni sehemu ambapo mfupa wa juu wa mguu unaungana na nyonga. # Nyonga ya Yakobo ikatenguka alipokuwa akishindana naye Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mwanamume alijeruhi nyonga ya Yakobo aliposhindana naye" # kwani kunakucha "jua litachomoza hivi karibuni" # umenibariki Hapa "umenibariki" ina maana ya kutamka baraka maalumu juu ya mtu na kusababisha mambo mazuri kutokea kwa huyo mtu. # sitakuacha uende mpaka uwe umenibariki Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya chanya. "Haiwezekani! Lazima unibariki kwanza, ndipo nitakuacha uondoke"