# Rundo hili ni shahidi kati yangu nawe leo Mawe hayawi mashahidi halisi kwa ajili ya mtu. "Rundo hili litakuwa ukumbusho kati yangu na wewe" # Galedi "Jina la Galedi lina maana ya "fungu la mashahidi" kwa lugha ya Yakobo. # Mispa "Jina la Mispa lina maana ya "mnara". # tunapokuwa hatuonani Hapa "nje ya macho" ina maana ya kutokuwa machoni pa mwenzako. "tutakapokuwa hatupo machoni mwetu sisi wawili" # japokuwa hakuna mwingine yupo nasi Hapa "nasi" ina maana ya Labani na Yakobo. "hata kama hakuna mtu wa kutuona" # tazama "kumbuka". Hii inaongeza msisitizo kwa kile kinachosemwa baadae.