# Labani akaambiwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mtu mmoja akamwambia Labani" # Siku ya tatu Ilikuwa utamaduni wa Kiyahudi kuhesabu siku ya kuanza safari kama siku ya kwanza. "Siku mbili baada ya kuondoka" # kwamba Yakobo amekimbia Yakobo pekee ndiye anayetajwa kwa sababu ndiye kiongozi wa familia. Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba familia yake ilikwenda naye. "ya kwamba Yakobo alitoroka na wake zake na watoto wake" # Hivyo akawachukua "Kwa hiyo labani akachukua" # na kumfuatia "na kumfukuza Yakobo" # kwa safari ya siku saba Labani alitumia siku saba akitembea kumfikia Yakobo. # Akampita "Alimfikia"