# Labani akamwambia "Labani akamwambia Yakobo" # Ikiwa nimepata kibali machoni pako Msemo wa "machoni pako" ni lugha inayomaanisha mawazo na maoni ya Yakobo. Iwapo nimepata kibali na wewe" au "Iwapo unapendezwa na mimi" # nimepata kibali Hii ni lahaja yenye maana ya mtu amekubalika na mtu mwingine. # subiri, kwa sababu "tafadhali kaa, kwa sababu" # nimejifunza kwa kutumia uaguzi "Nimegundua kwa desturi yangu ya kiroho na uchawi" # kwa ajili yako "kwa sababu yako" # Taja ujira wako Hii inaweza kuwekwa wazi. "Niambie nahitaji kukulipa kiasi gani kukuweka hapa"