# Mungu akamkumbuka Raheli na kumsikiliza Msemo huu "akamkumbuka" una maana kukumbuka. Hii haimaanishi Mungu alimsahau Raheli. Ina maana alimfikiria juu ya ombi lake. "Mungu alimfikiria Raheli na kumpatia kile alichokitaka" # Mungu ameiondoa aibu yangu Mungu kusababisha Raheli kutosikia aibu tena inazungumziwa kana kwamba "aibu" ni kitu ambacho mtu anaweza kukichukua kutoka kwa mtu mwingine. Nomino inayojitegemea "aibu" inaweza kuwekwa kama "kuona aibu". "Mungu amenisababishia nisione aibu tena" # Akamwita jina lake Yusufu "Jina la Yusufu maana yake ni "na aongeze" # Yahwe ameniongeza mwana mwingine watoto wa kwanza wa Raheli walitokana na mtumishi wa kike wa Bilha.