# watu wa mashariki Hii ina maana ya watu wa Paddani Aramu, ambayo ni nchi mashariki mwa nchi ya Kaanani. # na, tazama, makundi matatu ya kondoo yalikuwa yamelala kando yake Neno "tazama" linaweka alama ya mwanzo wa tukio lingine katika simulizi kubwa. # Kwani kutoka katika hicho kisima "Kwani kutoka katika kisima hicho". Msemo huu unaweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu jinsi wafugaji waliwanywesha mifugo" # wangeyanywesha "wafugaji wangewanywesha" au "wale waliokuwa wakitunza kondoo wangewanywesha" # mdomo wa kisima Hapa "mdomo" ni njia ya kuelezea uwazi. "uwazi wa kisima"