# Nao wakasema Hii ina maana ya Abimeleki, Ahuzathi na Fikoli. Mmoja wao aliongea na wengine wawili walikubaliana na kile alichosema. Haikumaanisha waliongea kwa wakati mmoja. "mmoja wao alisema" # Tumeona yakini "Tunajua" au "Tuna uhakika" # Hivyo na tufanye agano "Kwa hiyo tunataka kufanya agano" # na kama sisi tulivyokutendea vema wewe Hii inaweza kutafsiriwa kama mwanzo wa sentensi mpya. "Tumetenda mema tu kwako" # umebarikiwa na Yahwe Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yahwe amekubariki"