# Kisha Isaka akaenda Beersheba Hapa "kwenda juu" inaweza kumaanisha kwenda kaskazini. "Isaka aliondoka pale na kwenda Beersheba" # kuvidisha vizazi vyako "atasababisha vizazi vyako kuongezeka maradufu" au "atasababisha vizazi vyako kuwa wengi sana" # kwa ajili ya mtumishi wangu Abrahimu "kwa mtumishi wangu Abrahamu" au unaweza kuweka maana yote wazi zaidi. "kwa sababu nilimuahidi mtumishi wangu Abrahamu kuwa nitafanya hili" # Isaka akajenga madhabahu pale Unaweza kuweka wazi kwa nini Isaka alijenga dhabahu. "Isaka alijenga dhabahu pale kutoa sadaka kwa Yahwe" # akaliita jina la Yahwe "Kuita" ina maana ya kuomba au kuabudu. Hapa "jina" lina maana ya Yahwe. "aliomba kwa Yahwe" au "alimuabudu Yahwe"