# Hivyo Isaka akakaa Gerari Isaka pekee ndiye aliyetajwa kwa sababu ni kiongozi wa familia, lakini familia yake yote ilikuwa pamoja naye. "Kwa hiyo Isaka na familia yake walikaa Gerari" # Aliogopa kusema Hapa "aliogopa" ina maana ya hisia isiyofaa inayompata mtu wakati akipata tishio la kudhuriwa kwake au kwa wengine. "Aliogopa kusema" # wamchukue Rebeka "ili kwamba wamchukue Rebeka" # Tazama, akamwona Isaka Neno "tazama" linaonyesha ya kwamba kile alichokiona Abimeleki kilimshangaza. "Na alishangazwa kuona ya kwamba Isaka" # akimpapasa Rebeka Maana zaweza kuwa 1) alikuwa akimgusa kwa njia ambayo mume humgusa mkewake au 2) alikuwa akicheka na kuzungumza pamoja naye kwa namna ambayo mume huzungumza na mkewe.