# Taarifa ya Jumla: Yahwe anaendelea kuzungumza na Isaka # Nitauzidisha uzao wako "Nitasababisha uwe na uzao mwingi" # kama nyota za mbinguni Hii inazungumzia kuhusu uzao wa Isaka kana kwamba walikuwa sawa na idadi ya nyota. # mbinguni Hii ina maana ya kila kitu juu ya dunia ikijumlisha jua, mwezi na nyota. # mataifa yote ya dunia yatabarikiwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nitabariki mataifa yote ya dunia" # Abrahamu aliitii sauti yangu na kutunza maelekezo yangu, amri zangu na sheria zangu Misemo hii "alitii sauti yangu" na "kutunza maelekezo yangu, amri zangu na sheria zangu" zina maana moja. "Abrahamu alinitii na kufanya kila kitu nilichomuamuru kufanya" # aliitii sauti yangu Hapa "sauti" ina maana ya Yahwe. "Alinitii"