# akawa mwindaji hodari "akawa hodari katika uwindaji na kuua wanyama kwa chakula" # mtu mkimya "mtu wa amani" au"mtu asiyekuwa na mambo mengi" # aliye tumia muda wake akiwa katika mahema Hii inazungumzia kuhusu muda kana kwamba ilikuwa bidhaa ambayo mtu angetumia. "aliyebaki katika mahema sehemu kubwa ya muda" # Kisha Neno hili linatumika kuweka alama ya kubadili mwelekeo, kutoka katika simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Isaka na Rebeka. # Isaka akampenda Hapa neno "akampenda" ina maana "alimpendelea" au "kumpenda zaidi" # kwa sababu alikula wanyama ambao alikuwa anawinda "kwa sababu alikula wanyama ambao Esau aliwinda" au "kwa sababu alifurahia kula wanyama pori ambao Esau alikamata"