# Isaka akaenda kutafakari shambani jioni "jioni moja Isaka alitoka shambani kufikiri". Hii inaweza kuwa muda mrefu baada ya mtumishi na Rebeka kuondoka nyumbani kwake kwa maana walisafiri umbali mrefu. # Alipotazama akaona, natazama, kulikuwa na ngamia wakija! Hili neno "tazama" hapa linatumasha kusikiliza kwa taarifa ya kushangaza inayofuata. "Alipotazama juu akashangaa kuona ngamia wakija" # Rebeka akatazama "Rebeka akatazama juu" # akaruka kutoka kwenye ngamia "alishuka juu ya ngamia haraka" # akachukua shela yake akajifunika "Kwa hiyo alijifunika uso na shela yake". Hii ni ishara ya heshima na adabu kwa mwanamume atakayemuoa. Maana kamili inaweza kuelezwa wazi. # shela Kipande cha kitambaa kilichotumika kufunika kichwa cha mtu, mabega na uso.