# akainuka na kutoka kwa mkewe aliye kufa "akasimama na kuacha mwili wa mke wake" # watoto wa kiume wa Hethi Hapa "watoto" ina maana ya wale waliotokana na Hethi. "uzao wa Hethi" au "Wahiti" # miongoni mwenu Wazo hili linaweza kuelezwa kwa lugha ya eneo. "katika nchi yako" au "hapa" # Tafadhari nipatieni mahali "Niuzie sehemu ya nchi" au "Niruhusu kununua kipande cha nchi" # wafu wangu Kivumishi kidogo "wafu" kinaweza kuelezwa kama kivumishi au kitenzi. "mke wangu aliyekufa" au "mke wangu ambaye amekufa"