# Taarifa ya Jumla Malaika wa Yahwe anaendelea kuzungumza na Abrahamu. # mataifa yote ya dunia watabarikiwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mimi, Bwana, nitabariki watu wote wanaoishi mahali pote" # mataifa ya dunia Hapa "mataifa" ina maana ya watu wa matiafa. # umetii sauti yangu Hapa "sauti" ina maana ya kile ambacho Mungu alisema. "umetii kile nilichosema" au "umenitii" # Abraham akarejea Ni Abrahamu pekee aliyetajwa kwa sababu alikuwa baba, lakini imeonekana ya kwamba mwanawe alikwenda naye. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Abrahamu na mwanawe walirejea" # vijana "watumishi" # wakaondoka "waliondoka sehemu ile" # akakaa Beerisheba Ni Abrahamu pekee aliyetajwa kwa sababu alikuwa kongozi wa familia yake na watumishi wake, lakini imeonekana walikuwa pamoja naye. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Abrahamu na watu wake alikaa Beerisheba"