# Abraham pia akamlalamikia Abimeleki Maana zaweza kuwa 1) Abrahamu alikuwa akilalamika kuhusu kile kilichotokea au 2) "Abrahamu pia alimkaripia Abimeleki" # kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamekinyang'anya "kwa sababu watumishi wa Abimeleki walichukua kisima kimoja cha visima vya Abrahamu" # wamekinyang'anya kwake "kuchukua kutoka kwa Abrahamu" au "wamekitawala" # sijalisikia hadi leo hii "Hii ni mara ya kwanza nimesikia kuhusu jambo hili" # Abrahamu akachukua kondoo na ng'ombe maksai akampatia Abimeleki Hii ni ishara ya urafiki na ya kwamba Abrahamu amekubali kuweka agano na Abimeleki.