# Mungu akayafunua macho ya Hajiri Mungu kumfanya Hajiri aweze kuona kisima inazungumzwa kana kwamba alimfungua macho kihalisia. "Mungu alisababisha Hajiri kuona" au "Mungu alimuonyesha Hajiri" # kiriba "chombo kilichoundwa na ngozi" au "mfuko" # kijana "mvulana" au "Ishameli" # Mungu akawa pamoja na kijana Hapa msemo wa "akawa pamoja" ni lahaja ambayo ina maana ya Mungu alimsaidia au alimbariki mvulana. "Mungu alimuongoza mvulana" au "Mungu alimbariki mvulana" # akawa mwindaji "akawa na uwezo sana wa kutumia upinde na mishale" # akampatia mke "akapata mke"