# mia moja "100" # Mungu amenifanya nicheke Sara alikuwa akicheka kwa sababu alishangazwa na alikuwa na furaha. Hii inaweza kuwekwa wazi. "Mungu alinisababisha nicheke kwa furaha" # kila mtu atakaye sikia Kile ambacho watu wangesikia kinaweza kuwekwa wazi. "kila mtu asikiaye kuhusu kile Mungu amefanya kwangu" # Nani angesema kwa Abraham kwamba Sara atalea mtoto Hili swali la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hakuna ambaye angeweza kusema kwa Abrahamu ya kwamba Sara atalea watoto" # atalea mtoto Hii ni lugha ya upole ikimaanisha kunyonyesha watoto. "mnyonyeshe mtoto maziwa yake mwenyewe"