# Wakamwambia "Kisha wakamwambia Abrahamu" # akasema, "Hakika nitarejea kwako Neno "akasema" lina maana ya mwanamume ambaye Abrahamu alimwita "Bwana" katika 18:3. # majira ya machipuko "pale ambapo majira kama haya yatakapowadia mwaka kesho" au "muda kama huu mwaka kesho" # na tazama Neno "tazama" hapa linatutahadharisha kuwa makini kwa taarifa ya kushangaza inayofuata. # mlangoni pa hema "katika uwazi wa hema" au "katika kiingilio cha hema"