# vipimo vitatu kama lita 22 # mkate Mkate huu yawezekana ulikuwa umepikwa haraka katika jiko la moto. Inawezekana ulikuwa tambarare au duara kama mikate midogo midogo ya duara. # kwa haraka "mtumishi aliharakisha" # akaiandaa "kuukata na kuubanika" # siagi Hii ina maana ya sehemu ngumu ya maziwa yaliogandishwa. Inawezekana ilikuwa mtindi au jibini. # ndama aliye kwisha andaliwa "ndama aliyebanikwa" # mbele yao "mbele ya wageni watatu"