# Taarifa ya Jumla: Yahwe aliendelea kuzungumza na Abramu wakati Abramu alipokuwa akiota. # Nitahukumu Hapa "hukumu" ni lugha nyingine kwa kile kitakachotokea baada ya Mungu kutoa hukumu. "Nitaadhibu" # wataowatumikia Maana kamili ya kauli hii inawezwa kufanywa wazi. "ambao vizazi vyako watawatumikia" # mali nyingi Hii ni lahaja. "mali nyingi" au "utajiri mkubwa" # utakwenda kwa baba zako Hii ni njia ya upole ya kusema "utakufa" # baba Neno "baba" lina maana sawa na mababu. "mababu" # utazikwa katika uzee mwema "utakuwa mzee sana utakapokufa na familia yako itazika mwili wako" # Katika kizazi cha nne Hapa kizazi kimoja kina maana ya urefu wa miaka 100. "Baada ya miaka mia nne" # watakuja tena hapa "vizazi vyako watakuja hapa tena". Vizazi vya Abrahamu vitakuja katika nchi ampabo Abramu alikuwa akiishi, nchi ambayo Yahwe aliahidi kumpatia. # haujafikia mwisho wake "haijakamilika" au "itakuwa mbaya zaidi kabla sijawaadhibu"