# Akamwamini Yahwe Hii ina maana alipokea na kuamini kile Yahwe alichosema ni kweli. # akamuhesabia jambo hili kuwa mwenye haki "Yahwe alimhesabia imani ya Abramu kama haki" au "Yahwe alimchukulia Abramu kuwa na haki kwa sababu Abramu alimuamini" # Mimi ni Yahwe, niliye kutoa katika Uru Yahwe alikuwa akimkumbusha Abrahamu kile alichokuwa amefanya ili Abrahamu aweze kumjua Yahwe alikuwa na nguvu kumpatia Abramu kile alichomuahidi. # kuirithi "kukipokea" au "ili kwamba ukimiliki" # nitajua je Abramu alikuwa akiulizia ushahidi zaidi ya kwamba Yahwe atampatia ile nchi.