# Kisha, tazama Neno "tazama" linasisitiza ukweli ya kwamba neno la Yahwe lilikuja kwa Abrahamu tena. # neno la Yahwe likaja Lugha hii ina maana ya kuwa Mungu alizungumza. "Yahwe alizungumza ujumbe wake" # neno la Yahwe Hapa "neno" linawakilisha ujumbe wa Yahwe. "Ujumbe wa Yahwe" # Mtu huyu Hii ina maana ya Eliezeri wa Dameski. # atakaye toka katika mwili wako ndiye "yule utakayekuwa baba yake" au "mwana wako kabisa". Mwana wa Abramu atakuwa mrithi wake. # uzihesabu nyota "hesabu nyota" # ndivyo uzao wako utakavyokuwa Kama vile Abramu atavyoshindwa kuhesabu nyota zote, hataweza kuhesabu uzao wake wote kwa sababu utakuwa mwingi sana.