# Baada ya mambo haya "Mambo haya" ina maana ya pale ambapo wafalme walipigana na Abramu akamuokoa Lutu. # neno la Yahwe likamjia Lahaja hii ina maana ya Yahwe akazungumza. "Yahwe alizunguza ujumbe wake" # neno la Yahwe Hapa "neno" inawakilisha ujumbe wa Yahwe. "ujumbe wa Yahwe" # ngao ... thawabu Mungu alitumia sitiari hizi mbili kumwambia Abramu juu ya tabia yake na uhusiano wake na Abramu. # mimi ni ngao yako Wanajeshi hutumia ngao kujilinda kwa maadui zao. "Nitakulinda kama ngao" au "Mimi ni ngao yako kukulinda" # thawabu "malipo". Hii ina maana ya malipo yanayostahili kwa mtu. Maana mbili zaweza kuwa 1) "Mimi ni yote unayohitaji" au 2) "Nitakupa yote unayohitaji". # Abram akasema, "Kwakuwa hujanipatia "Abramu aliendelea kuzungumza na kusema, "Kwa kuwa umenipatia"