# Hawa wafalme watano wa mwisho waliungana pamoja Taarifa ya kwamba majeshi yao walikuwa pamoja nao inaweza kuwekwa wazi. "Wafalme hawa watano wa nyuma na majeshi yao waliungana" # miaka kumi na mbili walimtumikia Matukio katika mistari ya 4-7 yalitokea kabla ya mstari wa 3. Lugha yakoinaweza kuwa na namna ya kuonyesha hivi. # walimtumikia Kedorlaoma Inawezekana walitakiwa kumlipa kodi na kumtumikia jeshini. "walikuwa chini ya utawala wa Kedorlaoma" # waliasi "walikataa kumtumikia" au "walisitisha kumtumika" # walikuja na kuwashambulia Walifanya hivi kwa sababu wafalme wengine waliasi. # Warefai ... Wazuzi ... Waemi ... Wahori Haya ni majina ya makundi ya watu. # Ashteroth Karnaimu ... Hamu ... Shawe Kiriathaimu ... Seiri ...El Parani Haya ni majina ya sehemu. # El Parani iliyo karibu na jangwa Huu msemo unasaidia wasomaji kuelewa El parani ilikuwa wapi. Inaweza kutafsiriwa katika sentensi tofauti kama italazimu. "El Parani. El Parani ipo karibu na jangwa"