# Sasa Neno hili linatumika kuonyesha kitakachofuatia ni taarifa ya nyuma kumsaidia msomaji kuelewa matukio yatakayofuata. # Nchi haikuwatosha wote Hapakuwa na ardhi ya kutosha ya malisho na maji kwa ajili ya wanyama wao. # mali zao Hii inajumuisha mifugo, ambayo inahitaji malisho na maji. # hawakuweza kukaa pamoja "hawakuweza kuishi pamoja" # Wakanaani pamoja na Waperizi walikuwa wakiishi katika nchi ile wakati huo Hii ni sababu nyingine ya nchi kutoweza kuwahimili wote.