# Aliendelea na safari yake Abramu na familia yake walisafiri kwa hatua, kwenda kutoka sehemu hadi sehemu. Hii inaweza kufanywa wazi. "Waliendelea na safari yao" # mahali ambapo hema yake ilikuwa tangu mwanzo Watafsiri wanaweza kuweka maandishi machache yanayosema "Tazama Mwanzo 12:8." Muda wa safari yake unaweza kuwekwa wazi. "katika eneo alipotenga hema lake kabla hajakwenda Misri" # akaliitia jina la Yahwe "aliomba katika jina la Yahwe" au"alimuabudu Yahwe"