# Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Tera Sentensi hii inatambulisha habari ya vizazi vya Tera. Mwanzo 11:27-25:11 unazungumzia kuhusu vizazi vya Tera, mahsusi mwanae Abrahamu. "Hii ni habari ya vizazi vya Tera" # Harani akafa machoni pa baba yake Tera Hii ina maana ya kwamba Harani alikufa wakati baba yake akiwa hai. "Harani alikufa wakati baba yake, Tera, alipokuwa naye"