# Maelezo ya Jumla: Katika mistari ya 25-27 Nuhu anatamka laana juu ya mwana wa Hamu na baraka juu ya ndugu za hamu. Kile alichokisema Nuhu juu yao pia iliwahusu uzao wao. # Maelezo ya Jumla: Misemo tofauti katika mistari hii inakusudiwa kuonyesha ya kwamba hii ilikuwa shairi. # alipozinduka kutoka katika ulevi wake "akawa mtulivu" # mtoto wake mdogo Hii ina maana ya Hamu. "mwanawe mdogo, Hamu" # Alaaniwe Kanaani "Ninakulaani Kaanani" au "Na mambo mabaya yafanyike kwako Kaanani" # Kanaani Huyu alikuwa mmoja wa wana wa Hamu. "mwana wa Hamu Kaanani" # mtumishi kwa watumishi wa ndugu zake "mtumishi wa chini wa kaka zake" au "mtumishi mwenye umuhimu wa chini kabisa kati ya ndugu zake" # ndugu zake Hii inaweza kumaanisha ndugu zake Kaanani au ndugu zake kwa ujumla.