# Maelezo ya Jumla: Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu na wanawe. # ninalithibitisha agano langu pamoja nanyi "kwa kusema hivi, ninafanya agano langu pamoja na wewe" # mwili Maana zaweza kuwa 1) binadamu wote au 2) wenye viumbe wote, kujumlisha binadamu na wanyama. # Tena hapatatokea gharika ya kuangamiza nchi "Hakutakuwa tena na gharika ambalo litaangamiza nchi". Kutakuwa na gharika, lakini hazitaangamiza dunia nzima. # ishara Hii ina maana ya ukumbusho wa jambo lililoahidiwa. # agano ... kwa vizazi vyote vya baadaye Agano hili linamhusu Nuhu na familia yake na pia vizazi vyote vitakavyofuata.