# Hivyo kila kilichokuwa hai ... kilifutwa Ikiwezekana, hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kwa hiyo kila kiumbe hai ... kikatoweka" au "Kwa hiyo gharika iliangamiza kabisa kila kiumbe hai" # Vyote viliangamizwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu aliwaangamiza wote" # kutoka kwenye nchi "kwa hiyo hawakuwa katika nchi" # na wale waliokuwa naye "na watu pamoja na wanyama waliokuwa naye" # walisalia "walibaki" au "waliishi" au"walibaki hai" # Maji yalitawala nchi "Maji yenye kina kirefu yalifunika nchi yote" au "Maji yalibaki na gharika kubwa juu ya nchi"