# Taarifa ya jumla: Mistari ya 6-12 inarudia kwa mara ya pili na kutoa kwa utondoti jinsi gani Nuhu alivyoinbgia ndani ya safina na familia yake pamoja na wanyama katika 7:1. Hili sio tukio jipya. # Wanyama ambao ni safi Hawa walikuwa wanyama ambao Mungu aliruhusu watu wake kuwala na kuwatoa kama sadaka kwake. # wanyama ambao si safi Hawa walikuwa wanyama ambao Mungu hakuruhusu watu wake wale au kuwato kama sadaka kwake. # wawili wawili Wanyama waliingia kwenye safina katika makundi ya dume mmoja na jike mmoja. # Ikawa kwamba Msemo huu unatumika hapa kuweka alama kuhusu tukio muhimu katika simulizi hii. Mwanzo wa gharika. # baada ya zile siku saba "baadaya siku saba" au"siku saba baadaye" # maji ya gharika yakaja juu ya nchi Habari inayojitokeza, "ikaanza kunyesha" inaweza kufanywa kuwa wazi. "ikaanza kunyesha na maji ya gharika yakaja juu ya nchi"