# kwa jinsi yake "wa kila aina tofauti" # kitambaacho ardhini Hii inamaana ya wanyama wadogo ambao hutambaa juu ya ardhi # viwili vya kila aina Hii inamaana ya ain mbili ya kila aina ya ndege na mnyama. # viwe salama "ili uweze kuwaweka wawe hai" # kwako ... kwa ajili yako .. chako Hii inamaana ya Nuhu na ni katika umoja # chakula kinacholiwa "chakula ambacho watu na wanyama hula" # Kwa hiyo Nuhu akafanya hivi. kulingana na yote ambayo Mungu alimuagiza, ndivyo alifanya Sentensi hizi mbili zinamaanisha jambo moja. Sentensi ya pili inafafanua ya kwanza na kuweka msisitizo ya kwamba Nuhu alimtii Mungu. Sentensi hizi zilizo sambamba zinaweza kuunganishwa kuwa kitu kimoja. "Kwa hiyo Nuhu alifanya kila kitu alichoambiwa na Mungu kufanya"