# paa la safina Inawezekana hii lilikuwa paa lililochongeka au lililolala. Kusudi lake lilikuwa kulinda kila kitu ndani ya safina dhidi ya mvua. # dhiraa Dhiraa ilikuwa ni namba ya kipimo, kiasi kidogo tu kwa mita moja. # ya chini, ya pili na ya tatu "dari ya chini, ya katikati, na ya juu" au "dari tatu ndani" # dari "sakafu" au "daraja" # Sikiliza Mungu alinena hivi ili kusudi kusisitiza ya kuwa angefanya kile alichotarajia kukifanya. "Sikiliza" au "Sikiliza kile nachosema" # nimekaribia kuleta gharika ya maji "Nimekaribia kutuma mafuriko ya maji" au "ninakaribia kusababisha mafuriko" # mwili wote Hapa "mwili" inawakilisha viumbe vyote vya mwili, kujumlisha binadamu na wanyama. # wenye mwili wote wakaao ndani ya nchi wenye pumzi ya uhai Hapa "pumzi" inawakilisha uhai. "inayoishi"