# akawa baba wa Methusela "akapata mwana wake wa kiume Methusela" # Methusela Hili ni jina la mwanamume # Henoko akaenenda na Mungu Kuenenda na mtu ni sitiari ya kuwa na uhusiano wa karibu na yeye. "Henoko alikuwa na uhusiano wa karibu na Mungu" au "Henoko aliishi kwa umoja na Mungu" # Akawa baba wa wana zaidi wa kiume na kike "Akawa na wana zaidi wa kiume na kike" # Henoko aliishi miaka 365 "Henoko aliishi jumla ya miaka 365" # kisha alitoweka Neno "alitoweka" linamaanisha Henoko. Hakuwa duniani tena. # kwa kuwa Mungu alimtwaa Hii inamaana Mungu alimtwaa Henoko awe naye.