# Macho ya wote wawili yalifumbuliwa "Kisha macho yao yakafumbuliwa" au "Wakapata ufahamu" au "Wakaelewa" # Wakashona "wakakaza" au"wakaunganisha" # majani ya miti Iwapo watu hawajui majani ya miti yakoje, hii yaweza kutafsiriwa kama "majani makubwa ya mti" au kwa wepesi "majani makubwa" # na wakatengeneza vya kujifunika kwa ajili wao wenyewe Walifanya hivi kwa sababu walikuwa na aibu. Taarifa hii inayojitokea yaweza kufanywa dhahiri kama itahitajika. "na wakajivika navyo kwa sababu walikuwa na aibu" # majira ya kupoa kwa jua "katika kipindi hicho cha siku ambapo hewa tulivu huvuma" # kutoka kwa uwepo wa Yahwe Mungu "kuepuka uwepo wa Yahwe Mungu" au "ili kwamba Yahwe Mungu asiweze kuwaona" au "kutoka kwa Yahwe Mungu"