# Taarifa ya jumla Kinachofuata kimeandikwa na mwandishi. Mwanamume hakusema vitu hivi. # Kwa hiyo "Hii ni kwa sababu" # mwanaume atawaacha baba yake na mama yake "mwanamume ataacha kuishi kwenye nyumba ya baba na mama yake." Hii inahusu wanamume kwa ujumla. Hailengi mwanamume fulani katika muda fulani. # watakuwa mwili mmoja Lugha hii inaongelea tendo la ngono kana kwamba miili inakutana pamoja na kuwa kama mwili mmoja. "miili yao miwili itakuwa mwili mmoja" # Wote wawili walikuwa uchi Neno "walikuwa" linamaana ya mwanamume na mwanamke ambao Mungu aliwaumba. # uchi "kutovaa mavazi" # lakini hawakuona aibu "hawakuona aibu kwa kuwa uchi"